STARBOY’ Sio ya Wizkid Tena, ni mali ya The Weeknd.

Pop staa kutoka Canada ‘The Weeknd’ amefungua kesi dhidi ya kampuni ya Eymun Talasazan iliyokuwa na mpango wa kusajili jina la STARBOY kama Brand yao akidai kuwa neno hilo tayari ameshalilipia Usajili wake kwenye muziki na biashara pia.
Eymun Talasazan ilitaka kusajili kipindi cha Tv cha STARBOY siku 11 baada ya studio za MARVEL kuthibitisha ujio wa kitabu cha vikatuni cha STARBOY kitakachomuhusisha THE WEEKND, kitabu hichi kinatoka June 2018,
The Weeknd ana wimbo unaitwa ‘StarBoy’ huku Afrika, Nigeria kuna WizKid ni msanii mkubwa anayefahamika kama STARBOY.
Previous
Next Post »